Tanzania Industrial Research and Development Organization

TANZANIA INDUSTRIAL RESEARCH AND

DEVELOPMENT ORGANIZATION

ZIARA YA WAZIRI TIRDO


Posted On:04/3/2020WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa Mb alipotembelea Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) na kukagua shughuli mbalimbali za kitafiti na Maendeleo ya Viwanda zinazofanywa na Shirika hili, pia Mhe. Waziri ameridhishwa na hatua kubwa za kitafiti zenye matokeo chanya zinazofanywa na TIRDO. “Nimefurahishwa sana na tafiti mbalimbali zinazofanyika na wataalamu watafiti kutoka TIRDO, kwa kweli niwapongeze watafiti kwa kazi nzuri mnayoifanya endeleeni kubuni miradi itakayoendeleza au kuibua fursa za ukuzaji uchumi wa Viwanda Tanzania", alisema Waziri Bashungwa. Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa Mb alifurahishwa na mradi wa kuongeza thamani ya zao la muhogo ambapo aliona "bioethanol" na "biofertilizer" zinazozalishwa kutokana na mabaki ya taka za muhogo pia aliagiza kwamba TIRDO iangalie namna ya kuweza kuzalisha kwa wingi kwa ajili ya biashara ili iweze kuongeza mapato. Pia aliona dawa ya viuadudu (Vuruga) na aliagiza kwamba dawa hii iendelezwe ili ikasaidie wakulima wa pamba na mazao mengine ambayo yana changamoto kubwa ya wadudu na yanatumia fedha nyingi za kigeni kuagiza madawa nje ya nchi. Upande wa kuongeza thamani katika ngozi kwa kutumia malighafi za hapa nchini ameipongeza TIRDO na kuagiza kwamba TIRDO kupitia wataalamu wake wa teknolojia ya ngozi ihakikishe teknolojia hii inawafikia na kuwanufaishe wafugaji wetu ili kupata ngozi zenye ubora wa kutumika viwandani kutengeneza bidhaa za ngozi hapa nchini hii itapelekea pia kukuza pato la taifa na kuongeza ajira za wananchi wetu