emblem

TANZANIA INDUSTRIAL RESEARCH AND DEVELOPMENT ORGANIZATION

TIRDO for sustainable industrial development

News

MKAA MBADALA NI MKOMBOZI WA MAZINGIRA- PROF.M.A.MTAMBO

  • 2024-10-08 10:02:02

Article Image

Mkurugenzi Mkuu nwa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania Prof. Mkumbukwa Madundo Mtambo ameeleza namna mbavyo matumizi ya Mkaa mbadala unavyoweza kuokoa mazingira endapo wananchi watapata elimu juu ya matumizi ya mkaa mbadala. Prof.Mtambo ameyasema hayo katika kikao na waandishi wa habari uliowashirikisha wataalam kutoka TIRDO na Shirikalisilo la Kiserikali linalojihusisha na utafiti wa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii nchini -REPOA. Katika Mkutano huo, Prof. Mtambo ameeleza namna ambavyo taasisi hizo mbili zimeshirikiana kwa pamojqa katika kutoa elimu kwa wazalishaji wa mkaa mbadala toka mikoa 12 nchini ikiwashirikisha wazalishaji 58 ambao walipatiwa elimu juu ya uzalishaji bora wa Mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya mimea ambayo ni rafiki kwa mazingira. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa REPOA DR.Donald Mmari ameeleza kuwa ufadhili wao katika mradi huu umeleta manufaa makubwa ikiwa ni Pamoja ni kuwafikia wazalishaji wengi ambao mpaka sasa wanaendelea na uzalishaji wa mkaa mbadala katika mikoa hiyo 12. DR.Mmari ameongeza kuwa takwimu zinaonesha kati mwaka 2015 na mwaka 2022 kumekuwa na ongezeko la uharibifu wa mazingira kutoka hekta laki tatu na elfu kumi na mbili (312,000) mpaka zaidi ya laki nne na sitini na tisa (469,000) ambao ni ongezeko la asilimia ishirini na sita (26%) kwa kipindi cha miaka saba. Mratibu wa mradi huo kutoka TIRDO Bi. Kunda Sikazwe ambaye ni mtaalam mtafiti wa mazingira ameeleza kuwa changamoto iliopo kubwa ni uelewa wa jamii na upatikanaji wa mkaa huo katika maziringa rafiki kwa watumaiji. “Katika tafiti zetu tumegundua kuwa watu wanapenda kutumia huu mkaa lakini bado upatikanaji wake ni mdogo katika mazingira ya wananchi’’ aliongeza Bi.Kunda . Bi Kunda alieleza changamoto zingine kuwa ni mtizamo wa jamii juu ya mkaa huo, idadi ndogo ya wazalishaji Pamoja na ukosefu wa elimu kwa jamii juu ya manufaa ya kimazingira na kiafya kwa watumiaji na jamii kwa ujumla. Mtaalam huyo aliongeza kuwa wao kama watafiti wananendelea kutoa elimu na kuhamasisha wazalishaji zaidi kuongezeka ili kuweza kuwafikia watumiaji wengi kwa wakati mmoja. Mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya Mimemea(BIOMAS) unazalishwa kutokana na mabaki ya mimea kama vifuu vya nazi,vifuu vya chikichi, maranda ya mbao, mabaki ya mazao kama magunzi ya mahindi, maganda ya kahawa na pumba za mpunga. Akihitimisha mkutano hu , Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO Pof.Mkumbukwa Mtambo alitoa wito kwa wazallioshaji na watumiaji kwa ujumla kutumia mkaa mbadala ili kuokoa mazingira na afya ya watumiaji. Prof.Mtambo ameeleza kuwa TIRDO inawakaribisha wazalishaji kuja kupima mkaa wao katika maabara za TIRDO ili kuhakikisha kuwa mkaa unaokwenda kwa jamii ni safi na salama na unaokidhi matakwa ya kisheria juu ya afya ya mazingira na jamii kwa ujumla. Prof. Mtambo aliongeza kuwa waliweza kukusanya sampuli 42 na kati ya hizo waligundua karibu asilimia 50 hazikufikia viwango vinavyohitajika na ndipo TIRDO ilipoanza kutoa elimu na kuandaa mwongozo wa namna bora ya uzalishaji wa Mkaa huo. ‘’Pamoja na kuwa wazalishaji bado ni wachache lakini hata hao wachache bado kuna changamoto katika ubora wa mkaa wa na hivyo tunawakaribisha kuja kupata elimu ya namna bora ya kuzalisha mkaa bora kutoka kwa wataalam wetu na kuleta sampuli zao kupima katika maabara zetu’’ aliongeza Prof.Mtambo.