News
Mhe. Dkt. SELEMENI JAFO (Mb) ATEMBELEA TIRDO, AAGIZA UKAMILISHAJI MFUMO WA UTAMBUZI WA FURSA ZA VIWANDA NCHINI
-
2024-07-22 19:38:53
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Said Jafo (Mb) amefanya ziara ya kutembelea shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kuteuliwa katika Wizara hiyo tarehe 2 Julai 2024. Mhe. Dkt.Jaffo ametoa maagizo ya kukamilika kwa mfumo wa ukusanyaji na utambuzi wa fursa za Viwanda nchini (National Industrial Information Management System - (NIIMS) unaosimamiwa na TIRDO chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara katika mwaka huu wa fedha kabla ya kufika Juni 2025 ili taarifa hizo ziweze kuleta manufaa kwa sekta ya Viwanda na taifa kwa ujumla.