News
TIRDO NA STAMICO WASAINI MKATABA WA UTAFITI WA MADINI YA KIMKAKATI NCHINI
-
2025-11-12 11:32:04
Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) na Shirika la Mdini nchini (STAMICO) kwa pamoja wamesainiana mkataba wa wa awali (MOU) juu ya utafiti wa kiufundi katika kufanya utafiti wa madini ya Kimkakati katika mikoa ya Kagera na Singida. Katika uwasilishaji wa taarifa hiyo, Mkurugenzi mkuu wa TIRDO Prof.Mkumbukwa Madundo Mtambo amewaasa wataalam waliopewa jukumu hilo kuhakikisha wanafanya kazi kwa uweledi huku wakijua utafiti huu ni wa muhimu sana katika maendeleo ya Viwanda na sekta ya madini nchini. Prof.Mtambo ameongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imeikabidhi TIRDO jukumu la kuongoza utafiti mkubwa wa kitaifa ili kutathmini uwezo wa kiuchumi na viwandani wa rasilimali za madini ya mkakati. Madini haya ni muhimu kwa ujenzi wa viwanda na mageuzi ya uchumi. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Madini nchini DR. Venance Mwasse amesema kuwa wao kama wataalam wa madini watahakikisha malengo yanafikiwa na nchi inanufaika na utafiti huu, Dr.Mwasse aliongeza kuwa Ushirikiano kati ya TIRDO na STAMICO ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda nchini. Unaonyesha nguvu ya kuunganisha utafiti wa kisayansi, ubunifu wa kiteknolojia, na maendeleo ya rasilimali za madini. Ushirikiano huu utachangia kujenga sekta ya viwanda inayotegemea maarifa, ushindani, na uimara. Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uhandisi kutoka TIRDO Mha. Ramson Mwilangali amesema kuwa utafiti huo unaanza mara moja kuanzia sasa ambapo katika mkoa wa Singida utafiti utafanyika katika Wilaya na Kiomboi na kwa Mkoa wa Kagera utafiti huo utafanyika katika WEilaya ya Kyerwa. Mhandisi Ramson amezitaja madini ya kimkakati kuwa ni, Lithium inayotumika kutengeza betri za magari ya umeme.Cobalt – betri na vifaa vya elektroniki.Nickel – betri na chuma cha pua.Graphite – katodi za betri pampja na Manganese inayotumika katika uzalishaji wa chuma na betri. Upatikanaji wa takwimu sahihi wa madini ya kimkakati kwa ajili ya mamlaka za juu kufanya maamuzi ya uendelezaji ; Prof. Mtambo pia aliongeza kuwa utafiti huu utasaidia katika andiko la mradi ambalo litawawezesha upatikanaji wa fedha toka taasisi za kiefedha kwa ajili ya utekelezaji , Kuongeza chachu ya uendelezaji wa rasilimali za madini kwa ajili ya uchumi endelevu wa viwanda ,Kusaidia katika uendelezaji wa mnyororo wa thamani wa madini hayo hapa nchini na kuondoa dhana ya kusafirisha madini ghafi , Kupanga kwa ufanisi na kusimamia kwa uwajibikaji utajiri wa madini wa Tanzania kwa maendeleo ya muda mrefu ya nchi Kuongeza ajira na ustawi wa jamii katika sehemu husika pamoja na uboreshaji na uendelezaji wa miundombinu kama barabara, umeme, maji, n.k pamoja na. Pamoja na TIRDO, STAMICO lakini pia utafiti huu utahisha pia wataalam kutoka Shule ya Madini na Jiolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mkutano huu umeonyesha kiwango cha juu cha utaalamu, ushirikiano, na kujitolea katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya taifa letu. Majadiliano, hoja, na mawasilisho yaliyowasilishwa yameimarisha mipango yetu ya kiufundi na kuweka msingi thabiti kwa utekelezaji wenye mafanikio wa mradi huu muhimu kwa taifa. Mkataba huo wa ushirikiano umefikiwa mjini Morogoro katika ukimbi wa chuo cha Ujenzi ambapo kwa pamoja washiriki wote wamekubaliana kuanza kazi mara moja kwa kuzingatia maelekezo ya viongozi lakini pia kuhakikisha kuwa taifa linanufaika na rasilimali zilizopo nchini baada ya utafiti wa kina wa kitaalam.

