emblem

TANZANIA INDUSTRIAL RESEARCH AND DEVELOPMENT ORGANIZATION

TIRDO for sustainable industrial development

News

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo yaitembelea TIRDO

  • 2024-03-19 12:32:10

Article Image

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala katika Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) ambalo linatarajiwa kumalizika June 30,2024. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) amesema serikali imeiongezea uwezo wa kimiundombinu upande wa vifaa na sasa jengo Shirika la TIRDO ili kuweza kutoa huduma bora kwa viwanda na kuendeleza atamizi mbalimbali shirikani. Aidha Kamati hiyo imeiomba serikali kupitia Wizara kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa kutenga na kutoa bajeti iliyobakia. Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)amesema kwa hatua zilizobaki kukamilisha ujenzi wa jengo hilo, TIRDO ilitengewa bajeti ya shilingi bilioni 3.4 ambapo mpaka sasa wameshapokea shilingi bilioni 1.54 kwaajili ya ukamilishani wa jengo hilo. Mhe. Waziri ameishukuru Kamati hiyo kwa kuweza kuisukuma serikali na hatimae kupatikana kwa fedha hizo na ujenzi ukiendelea kutoka asilimia 50 iliyokuwepo mwaka jana na kufikia asilimia 72 kwasasa