emblem

TANZANIA INDUSTRIAL RESEARCH AND DEVELOPMENT ORGANIZATION

TIRDO for sustainable industrial development

News

TIRDO YAIKABIDHI CAMARTEC MATAMBO WA KUMENYA GANDA LAINI LA KOROSHO.

  • 2024-03-29 11:04:02

Article Image

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC), Mtambo wa kumenya ganda laini la korosho katika karakana za TIRDO. Hii ni katika jitihada za kuanzisha kiwanda darasa cha kuchakata zao la korosho mkoani Singida, ambapo mbali na kubangua korosho kitatumia mashine hii ya kisasa kumenya ganda la ndani pamoja na kuzitenga korosho katika daraja za ubora. Kiwanda darasa hicho kinategemewa kuchochea uanzishwaji wa viwanda vingine vya aina hiyo katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kutekeleza jukumu hili CAMARTEC inashirikiana na TIRDO, TEMDO na SIDO.